Swahili

Swahili | Kiswahili

The State Emergency Service (Huduma ya Dharura ya Jimbo) (SES) ni shirika la kujitolea ambalo linaweza kukusaidia katika dharura ya mafuriko au dhoruba. Huna haja ya kulipia huduma hii.

Ukipiga 132 500 kutoka kwenye simu yako, watu wanaojitolea kutoka SES watakuja nyumbani kwako ikiwa nyumba imefurika au kuharibiwa na dhoruba. Unaweza pia kuomba mkalimani. Wafanyakazi wa kujitolea wa SES daima huvaa sare ya rangi ya chungwa. Wana uzoefu katika kukabiliana na mafuriko na dharura za dhoruba.

Tafadhali tazama hapa chini kwa habari zaidi kuhusu jinsi unavyoweza kuandaa familia yako na nyumba yako kwa mafuriko na dhoruba.

Ikiwa huelewi habari hii, waulize mwanafamilia, rafiki au jirani kwa usaidizi.

Ujumbe wa jumla

Dharura zinaweza kutokea mahali popote, wakati wowote.

Kwa kujitayarisha kwa ajili ya dharura, unaweza kupunguza athari za dharura, na kupona haraka baadaye.

Tunataka kuhakikisha kwamba watu wote wa Victoria wamejitayarisha na kujua la kufanya iwapo maeneo ya karibu yao yameathiriwa na dhoruba au mafuriko.

Iwapo unahitaji mkalimani akusaidie kwa maelezo ya dharura, pigia the Translating and Interpreting Service (Huduma ya Utafsiri na Ukalimani) kwa 131 450 (simu ya bure) na uwombe wakupigie simu VicEmergency Hotline (1800 226 226).

Ikiwa unamfahamu mtu ambaye hawezi kuzungumza Kiingereza, mpe nambari hii.

Jihadhari baada ya dharura, kwani hatari bado zinaweza kuwepo.

Huenda isiwe salama kwako kurudi nyumbani kwako au mahali pa kazi.

Pata habari - fuatilia maonyo ya dhoruba na mafuriko kupitia simu ya dharura ya VicEmergency (1800 226 226) au kwenye tovuti ya VicEmergency - https://emergency.vic.gov.au/respond/

Dhoruba Maalum

Dhoruba zinaweza kutokea mahali popote na wakati wowote.

Zinaweza kuleta upepo mkali, mafuriko ya ghafla, mvua ya mawe makubwa na umeme.

Zinaweza kusababisha uharibifu mkubwa na kuweka maisha yako hatarini.

Iwapo unahitaji mkalimani akusaidie kwa maelezo ya dharura, pigia the Translating and Interpreting Service (Huduma ya Utafsiri na Ukalimani) kwa 131 450 (simu ya bure) na uwombe wakupigie simu VicEmergency Hotline (1800 226 226).

Panga kile utakachofanya na utakachopeleka, ikiwa unahitaji kuhama.

Jua jinsi ya kuandaa nyumba yako na/au mahali pa kazi, na nini cha kufanya wakati wa dhoruba kwenye tovuti ya VICSES – www.ses.vic.gov.au

Flood Audio
Flood audio coming soon
Storm Audio
StormSafe audio coming soon